Kamishna mkuu wa zamani wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ataongoza uchunguzi wa wazi juu ya ukiukwaji wa kimfumo huko Israel na maeneo ya Palestina.
Rais wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa amesema kuwa Pillay, ataongoza jopo la watu watatu kuchunguza unyanyasaji na sababu za msingi katika mzozo huo wa karne.
Uchunguzi huo ulipata nguvu wakati wa kikao maalumu kilichofanyika Mei 27 kujadili ongezeko la vurugu kubwa baina ya Waisrael na Wapalestina mapema mwezi huo.
Ghasia hizo ziliwaua Wapalestina 260 na Waisrael 13. Uchunguzi huo unalenga kuangalia zaidi sababu zote za msingi za mivutano ya mara kwa mara, ukosefu wa utulivu, ubaguzi wa kimfumo na ukandamizaji.

No comments:
Post a Comment