Search This Blog

Tuesday, July 20, 2021

Jeshi la polisi Kinondoni limemuua mtu mmoja anayedaiwa ni jambazi baada ya kupora simu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemuua mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi baada ya kumpora simu mama aliyekuwa akitembea kwa miguu.

Akizungumza na Mwananchi Kamanda wa Polisi, Ramadhan Kingai amesema tukio hilo limetokea Jumatatu Julai 19, 2021 saa tatu kasoro wakati watu hao wakiwa na pikipiki eneo eneo la Kinondoni jirani na Dar Free Market.

Amesema baada ya tukio hilo watuhumiwa hao walianza kukimbia huku wakifyatua risasi bila kujua kama eneo hilo kulikuwa  na askari jirani.

"Walikuwa watu wawili kwenye pikipiki aina ya boxer baada ya kupora simu, walianza kukimbia huku wakifyatua  risasi ovyo askari wetu waliwakimbiza na kufanikiwa kumpiga risasi mmoja wao ambaye alidondoka chini," amesema Kamanda Kingai.

Amesema  katika tukio hilo walifanikiwa kupata pikipiki ania ya boxer yenye namba  pamoja na bastola aina ya brown ambayo usajili wake bado haujapatikana.

"Pamoja na kuipata pikipiki tumeafanikiwa kupata simu mmoja iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu, simu iliyoibwa pamoja na mtuhumiwa mmoja tunaendelea kumtafuta,"amesema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...