Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amewasimamisha kazi wakurugenzi watendaji wa halmashauri za Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja na mmoja wa Manispaa ya Mjini.
Ametangaza uamuzi huo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akifanya majumuisho ya ziara yake aliyofanya katika mikoa mitatu ya Unguja.
Dk Mwinyi amesema amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri hizo.
"Kwakweli niseme sijaridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri zote, hakuna yenye unafuu, kwahiyo naagiza wakurugenzi wote wasimame kazi kuanzia Sasa, ila naambiwa kuna halmashauri ambazo wakurugenzi wake wanakaimu hao siwagusi," amesema Dk Mwinyi
Halmashauri hizo ni Kusini, Kati, Kaskazini A, B na Manispaa ya Mjini Magharibi B.

No comments:
Post a Comment