Ujenzi wa maabara kwa ajili ya somo la biolojia kwa vitendo katika shule za sekondari ya Baray Khusumay, Endala uko katika hatua nzuri.
Ujenzi wa maabara katika shule hizo unatarajia kumalizika mwanzoni wa mwezi wa nane, serikali imetoa fedha kwa ajili ya kusaidia kumalizia ujenzi wa maabara hizo.
Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akitembelea ujenzi wa miundo mbinu katika kata ya Endamarariek. Mh. Kayanda amesema ujenzi wa miundo mbinu ya elimu lazima uendane na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.
Ameongeza kusema usimamizi wa matumizi ya fedha lazima uwe mzuri ujenzi wa maabara katika shule ya Baray Khusumay umebakia kutengeneza mfumo wa gesi na mfumo wa maji ili kukamilika.
Kuhusu ujenzi wa maabara ya sekondari ya Endala upo katika hatua ya uwekaji wa palasta nje na ndani ya maabara na kuweka mifereji. Kila shule imetengewa kiasi cha million 30 kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo ya maabara.
Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ametembelea shule za msingi Shauri Awaki na Manusay ambazo serikali imetoa kiasi cha million 12.5 kwa kila shule kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa.
Mh. Kayanda amesema ujenzi wa majengo ya madarasa lazima ujengwe kwa muongozo wa ujenzi wa serikali ambao unaonesha vipimo vya ujenzi wa madarasa. Ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa utakamilika mwanzoni mwa mwezi wa nane.
Ukamilishwaji wa vyumba vya madarasa utapunguza msongamano wawanafunzi. Mh. Kayanda amepongeza kamati za ujenzi za shule zinazosimamia ujenzi wa madarasa katika shule hizo.





No comments:
Post a Comment