Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

CHAMP: Fahamu silaha ya Marekani kujilinda dhidi ya makombora ya nyuklia kutoka Korea kaskazni


Wakati vita vya maneno kati ya Marekani na Korea kaskazani viliposheheni chini ya utawala wa rais Donald Trump , Marekani ilikuwa imeanza kuhisi joto la rais Kim Jong Un wa taifa hilo na kuanza kujiandaa kwa lolote lile .

Kando kando ya mji wa Albuquerque, katika jimbo la New Mexico , kundi moja la wataalam kutoka jeshi la angani la Marekani lilikuwa linatengeneza silaha ilio na malengo kadhaa : Kuzuia shambulio la kinyukllia la Korea kaskazini..

Silaha hio sio ya kawaida, ni silaha inayotumia mawimbi ya kielektroniki ambayo hayawezi kuwaathiri binadamu na inatumia teknolojia kama ile iliotumika kutengeneza tanuri ya Microwave.

Na kulingana na wataalamu kadhaa kuhusu masuala ya kijeshi waliozungumza na BBC Mundo , lengo lake kuu ni kuyafanya makomboya ya kinyuklia ya Korea kaskazini kushindwa kufanya kazi bila kufanya uharibifu.

Silaha hiyo imepatiwa jina la Microwave Interference Electronically High Power (CHAMP) na kwa msingi lengo lake ni kutoa mawimbi kutoka anga za juu yanayoweza kukaanga mifumo ya kielektroniki.

" Kwa kuzingatia hali ya teknolojia katika ulimwengu wa kisasa, ambapo karibu kila kitu hufanya kazi kwa njia ya kidijitali, aina hii ya kombora hutoa mawimbi makali ya kielektroniki yenye uwezo wa kukatiza au kufanya vifaa vya kielektroniki visifanye kazi, "kulingana na msemaji wa Kambi ya wanajeshi wa angani ya Kirtland huko Albuquerque..

Kambi hiyo ambayo ilikuwa mojawapo ya maeneo ya kutoa usaidizi kwa mradi wa kujenga bomu la atomiki wakati wa vita ya pili ya dunia , sasa inafanya utafiti kuhusu silaha hii mpya itakayotumia mawimbi ya kielektroniki.

" Silaha hiyo ya CHAMP ambayo ni kombora la masafa marefu lakini bila betri ya kulichaji, linaweza kurushwa kutoka ndege ya kivita aina ya B-52 , na linaweza kuruka umbali wa 1 . 127 kilometers , " kulingana na Fisher.

Lakini uzuri wake kama silaha ni zaidi ya shambulio la kiatomiki kutoka Korea kaskazini.

Silaha zinazotumia mawimbi ya kielektroniki

Hii sio mara ya kwanza kwa Marekani kutengeneza kombora kwa kutumia mawimbi ya kielektroniki.

Sharon Weinberger, muhariri mkuu wa sera ya kigeni alielezea BBC Mundo kwamba jeshi la angani limechunguza na kutumia mawimbi ya kielektroniki kama silaha miongo miwili iliopita

Kulingana na mtaalamu huyo , kifaa cha kijeshi kinachotumia mawimbi ya kielektroniki kilitumika nchini Afghanistan na Iraq kwa lengo la kulemaza mabomu na ndege zisizikuwa na rubani.

Lakini uzoefu wa jeshi la Marekani wa kutumia mabomu yanayotumia mawimbi ya kielektroniki ulianza miongo kadhaa iliopita.

Kitengo cha Pentagon , kinachofanya tafiti endelevu za kijeshi , kiliagizwa mwaka wa 1960 kuchambua madhara ya mawimbi ya kielektroniki kwa wanadamu.

"Yote hayo yalianza baada ya serikiali ya Muungano wa Usovieti kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Moscow kwa kutumia bomu la aina hiyo'', anaelezea Weinberger , mwanzilishi wa 'Imaginaries of war', dharura ya Pentagon iliobadili ulimwengu. ".

Matukio hayo yaliofanyika ndio yaliosababisha utafiti wa mawimbi hayo uliofanywa na jeshi la angani ambalo liliwatumia tumbili ili kuweza kubani athari ya bomu hilo kwa bindamu.

Lakini licha ya utafiti huo dhidi ya binadamu kufeli, utengenezaji wa silaha kwa kutumia teknolojia hiyo umechukua mkondo mpya katika miaka ya hivi karibuni.

Tumbili hao walitumiwa kupima athari ya mionzi hiyo ya kielektroniki .

Ijapokuwa makombora ya mawimbi ya kielektroniki yaliorushwa kutoka kwa ndege hayajatumiwa katika vita vya ardhini, vipimo vilivyofanywa vimeifanya idara ya ulinzi ya Marekani kuhisi kana kwamba kuna mafanikio na matokeo hayo.

Ijapokuwa wataalamu wanahakikisha kwamba vipimo kadhaa vimefanyika ili kuthibitisha uwezo wake , kufikia sasa idara ya ulinzi ina maelezo kuhusu moja.

Jaribio la kwanza Iilifanyika katika jangwa la Utah 2012, miaka mitatu tu baada ya uchunguzi wa kwanza kuhusu aina hiyo ya silaha kuanza rasmi katika maabara ya jeshi la wanaanga katika kambi ya Kirtland.

Kulingana na Fisher , mwezi Oktoba mwaka huo, ndege aina ya B-52 ilifyatua kombora linalotumia mawimbi ya kielektroniki katika jangwa eneo lenye ukubwa wa kilomita 4,000.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...