Staa wa filamu Aunty Ezekiel ametoa comment yake kwa Wema Sepetu kupost matangazo ya waganga kwenye page yake ya Instagram kwa kusema kuna maisha baada ya ustaa na mashabiki wanatakiwa watambue hilo.
Aunty Ezekiel amenena hayo baada ya baadhi ya mashabiki kutokea jamhuri ya watu wa mitandaoni hasa wa Instagram kumshambulia Wema Sepetu kupost matangazo hayo huku wakidai anashusha brand yake.
"Mimi nadhani ifike time watu wajue kuna maisha baada ya ustaa, mtu anaona kuna fursa ya kufanya kitu na akapata pesa kwanini asifanye kwa sababu hata yeye ni binaadam kama walivyo wengine wanaongea wanaona yao yamekwama wamuache afanye matangazo sidhani kama ni shida" amesema Aunty Ezekiel
Pia Aunty Ezekiel ametaja sifa za marafiki zake wa karibu kwenye tasnia ya filamu kama Irene Uwoya, Shamsa Ford na Wema Sepetu, zaidi akiongelea hilo tazama hapo chini kwenye video.

No comments:
Post a Comment