Search This Blog

Saturday, July 24, 2021

Anna Mghwira kuzikwa Jumatatu Arusha


Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Arusha Jumatatu Julai 26 mwaka huu.

Mghwira alifariki dunia jana Julai 22 katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Julai 23, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema mkoa huo umebeba jukumu la kuandaa mazishi ya Mghwira.

"Taarifa za awali ni kwamba tutampumzisha mama Anna Mghwira kwenye makazi yake ya milele Julai 26 mwaka huu jijini Arusha siku ya Jumatatu, taratibu za mazishi kwa sasa zinaendelea,"amesema Kagaigai.

Mghwira ambaye alikuwa mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2015 aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kuwa mkuu wa Mkoa huo mwaka 2017 akitokea chama cha ACT Wazalendo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...