Search This Blog

Thursday, June 3, 2021

Zarina Hassan aiomba jamii iwasaidie watoto wa kike wapate taulo

 


Mjasiriamali Zarina Hassan  ameiomba jamii iwasaidie watoto wa kike wapate taulo za kujisitiri wakati wanapokuwa kwenye hedhi.

Zari ametoa rai hiyo jana Jamatano alipokuwa kwenye hafla ya kugawa taulo hizo kwa shule za sekondari na msingi za mkoa wa Dar es Salaam.

Zari The Boss Lady ambaye pia ni mzazi mwenzake na msanii ‘Diamond Platnumz’, amesema si lazima kwa mtu atoe taulo nyingi bali anaweza kutoa hata mbili kulingana na uwezo wake.

Amesema ni vema jamii ikajenga utamaduni wa kuona jukumu hilo ni lao badala ya kuwaachia wachache.

"Kutoa ni moyo si utajiri, tujenge utamaduni wa kutoa hata kama ni kidogo kwakuwa kufanya hivyo tunakuwa tumemsaidia mtoto wa kike kutimiza ndoto zake” amesema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...