Search This Blog

Sunday, June 27, 2021

Yusuph Manji ndani ya mkutano mkuu wa Yanga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji ameteka mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Jumapili Juni 27, 2021 baada kutinga ukumbini.

Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa DYCC mkoani Dar es Salaam na Manji aliwasili saa 11:07 asubuhi huku msafara wake ukiwa na gari mawili aina ya Nissan Xtrail na Toyota Land Cruiser.

Baada ya gari hizo kuwasili wanachama walikuwa hawajui yupo katika gari gani lakini Manji alishuka kwenye Nissan Xtrail na mamia kuanza kumshangilia.

Si kumshangilia pekee, baadhi ya wanachama hao walifungua mlango wa gari hilo na Manji aliposhuka walianza  kupiga naye picha  huku mwenyewe akitabasamu na kufurahia kitendo hicho.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga alitoa nafasi ya kila aliyehitaji apige naye picha lakini baadhi ya walinzi waliopo ukumbini hapo kuhakikisha usalama unakuwa imara waliwazuia baadhi ya wanachama.

Baada ya kupiga picha kadhaa Manji aliingia katika ukumbi huo na kuibua shangwe kutoka kwa mamia ya wanachama.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...