Search This Blog

Tuesday, June 15, 2021

Yanga yaingia anga za kiungo huyu Mcongo

 


MERCEIL Ngimbi Vundi, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya AS Maniema Union anatajwa kuwa Kwenye rada za Yanga inayonolewa  na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi.

Nyota huyo aliletwa duniani Aprili 18,1997 ana umri wa miaka 24 ni raia wa Congo.

Habari zimeeleza kuwa kila kitu juu ya usajili wa nyota huyo kimekamilika hivyo wapo kwenye majadiliano ya mwisho kati ya Yanga na mchezaji mwenyewe.

"Muda na wakati wowote Ngimbi atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuicheza Klabu ya Yanga hii ni baada ya kufikia muafaka mzuri na viongozi wa Yanga.

"Tayari Ngimbi amewaambia mabosi wa Maniema kwamba anataka kwenda Yanga. Ni kati ya viungo bora sasa nchini kama usajili wake utakamilika basi watakuwa wamepata kiungo mzuri," ilieleza taarifa hiyo.

Kuhusu suala la usajili, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Injinia Hersi Said hivi karibuni alisema kuwa wamepanga kufanya usajili bora na wa kisasa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...