Search This Blog

Sunday, June 6, 2021

Waziri mkuu Majaliwa awaasa wananchi wa Lindi kutumia fursa zinazo wazunguka



Na  Ahmad Mmow,  Lindi. 

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi kutumia fursa zinazowazunguka ili kupandisha uchumi wao, mkoa huo na taifa.

Waziri mkuu Majaliwa ametoa wito huo leo mjini Lindi wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo wa mkoa wa Lindi.  

Waziri mkuu Majaliwa alisema iwapo wananchi wa mkoa huo watumia fursa zilizopo mkoani humo kikamilifu wataweza kuinua kiwango cha uchumi wa mtu mmoja mmoja, mkoa na taifa.

Alizitaja sekta za kilimo na mifugo kuwa ni miongoni mwa fursa zilizopo mkoani humu ambazo zikitumiwa vema zitainua uchumi. 

Waziri Majaliwa ambaye aliweka wazi kwamba fursa hizo zinaweza kuwa na tija kwa kufanyakazi kwa bidii juhudi na maarifa na kila mmoja akitimiza wajibu wake alisema mkoa wananchi wakijikita na kupewa ushirikiano wa kutosha katika sekta za kilimo na mifugo watanufaika. 

Aidha alibainisha fursa nyingine ambazo licha ya kuwepo lakini bado hazijawatumika na haziwanufaishi wananchi. Ikiwamo fukwe, vivutio vya utalii, bahari. 

Kwakuzingatia ukweli huo, waziri mkuu amezitaka halmashauri ziongeze usimamizi kwenye sekta ambazo zinafanywa kila siku, hasa ya kilimo. Huku akiwataka pia viongozi wa mkoa na wilaya za mkoa wa Lindi kusimamia sekta hizo kikamilifu. 

Waziri mkuu kwa masitiko alisema licha yakuwa na fursa nyingi ikiwamo vivutio vya utalii lakini havijatangazwa vyakutosha kiasi cha kuvutia watalii kwa wingi. Kwani mkoa huu kwa mwaka unatembelewa na watalii 3,800 tu. 

 '' Mitema imekufa, nani ameua, kwanini na nani ameuwa? Bahari haijatumika ipasavyo. Namkoa huu una fursa nyingi sana. Kuanzia Sudi, Mitema, Simaya, Nang'oma, Nkulukala, Kera nakadhalika. Wataalamu mpo wa kuwaongoza. Uvuvi pia haujakaa vizuri, wavuvi ni wachache kwa mkoa mzima kuna wavuvi 11,500 tu,'' alisema waziri mkuu. 

Mbali na hayo waziri mkuu amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Lindi kwamba mradi wa kuchakata gesi asilia ( NLG ) ambao mtambo wake unatarajiwa kujengwa katika manispaa ya Lindi, mitaa ya Mtokamkavu na Likong'o utaanza kutekelezwa hivi karibuni.  

Alisema moja ya miradi ya kimkakati ya serikali ya awamu ya sita ni mradi huo. Nakwamba hivi sasa kuna timu ya majadiliano inaendelea kufanya majadiliano. Lengo likiwa nikufanya uwe na tija kwa wananchi hao wa maeneo yatakayo jengwa mtambo huo, mkoa na taifa. Huku akibainisha vipengele vingi vimejadiliwa na bado vichache. Kwani hadi sasa vipengele 28 vimeshajadiliwa. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...