Search This Blog

Sunday, June 13, 2021

Wazazi Waaswa kutoa taarifa kama hawatarajii kuwapeleka watoto wao kwenye shule za Serikali

Serikali imewaasa wazazi wenye watoto waliopata ufaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye shule za Serikali hapa nchini kuhakikisha wanatoa taarifa za watoto wao mapema kama hawatarajii kujiunga na shule hizo kwani wapo wanafunzi ambao wamefaulu lakini hawakupata nafasi za kujiunga na shula za Serikali.

Akiongea na wananchi wa Kata ya Ziba katika shule ya sekondari Ziba hiyo jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema jumla ya wanafunzi 86,896 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano lakini wanafunzi takibani 3,800 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha tano kutokana na uhaba wa nafasi hizo, hivyo itakuwa vema kama wazazi na walezi wa wanafunzi waliopata nafasi kwenye shule za Serikali lakini hawataki kuwapeleka watoto wao huko watoe taarifa ili wale waliokosa nafasi wapate kuendelea na masomo kidato cha tano.


“ninachotaka kusisitiza kwa wazazi na walezi kwa sababu tuna wanafunzi kam 3,800 ambao hawajapata ya kuendelea na elimu ya ya kidato cha tano, kwa hivyo kama mzazi au mlezi ameshafanya maamuzi ya kumpeleka motto wake kwenye shule ya sekondari binafisi tunaomba ajaze fomu katika mfumo wetu ili aweze kuiachia nafasi hii kwa vijana ambao wamefaulu lakini wamekosa nafasi” ,alisema Waziri ummy Mwalimu.   

Aidha, Waziri Ummy Mwalimu ameahidi kupeleka fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa bwalo la kulia chakula katika shule ya sekondari Ziba ili kuondoa kero inayowakabili wanafunzi wa shule hiyo.

Naye mbunge wa Manonga Seif Gulamali amesema jumla ya shule 15 za msingi na 13 za sekondari zimepatiwa fedha na Serikali mwaka huu kiasi cha shilingi milioni 807 kujenga miundombinu mbalimbali pia mapema Julai Mosi, 2021 wanatarajia kupokea shilingi milioni 700 kwa ajili ya kujenga shule ya wasichana ambayo itakuwa imekamilika kwenye miundombinu yote na ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia suluhu Hassan katika kuendelea kuwajali wananchi kote nchini.  

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...