Watu 53 wamepoteza maisha baada ya watu wenye silaha kushambulia wakulima nchini Nigeria.
Kulingana na polisi katika jimbo la Zamfara, wezi wa ng'ombe waliwafyatulia risasi wakaazi na kuwashambulia wakulima wa eneo hilo.
Wakati watu 53 wakiwa wamepoteza maisha katika tukio hilo, hatua za usalama zimeongezwa katika jimbo hilo.
Washambuliaji walifyatua risasi wakiwa wamepanda kwenye pikipiki.

No comments:
Post a Comment