Viongozi wa mataifa tajiri yaliyostawi kiviwinda G7 hapo jana Jumamosi waliikabili China na tishio la magonjwa ya milipuko wakati mataifa hayo tajiri yakitangaza umoja mpya wa mataifa ya Magharibi katika mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana tangu 2019.
Rais wa Marekani Joe Biden na wenzake wanatarajiwa kuahidi msaada zaidi wa kifedha kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Nchi saba tajiri duniani za G7 zinaunga mkono hatua za pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaojadili swala la mabadiliko ya tabia nchi COP26 utakaofanyika nchini Scottland mnamo mwezi Novemba.
Mradi wao wa "Build Back Better World" unakusudia kushindana na mradi wa China wa kujenga miundombinu duniani, ambao umekosolewa sana kwa kuziweka nchi zinazoendelea katika madeni makubwa.
Viongozi wa Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani leo Jumapili watatoa tamko la pamoja juu ya mkutano wao.

No comments:
Post a Comment