Search This Blog

Tuesday, June 29, 2021

Utafiti wabaini kuchanganya dozi za chanjo kunaleta ufanisi


Njia ya kuchanganya chanjo za Covid - kwa kutumia chapa mbalimbali za chanjo ya Covid kwa dozi ya kwanza na ya pili - inatoa kinga nzuri dhidi ya virusi vya janga hilo, utafiti wa Uingereza umebaini

Majaribio yalitazama ufanisi wa dozi mbili za Pfizer, AstraZeneca na Mchanganyiko wote ulifanya kazi vizuri, ikitoa kinga ya mwili.

Ujuzi huu unaweza kupokea mazingira ya chanjo inayotolewa, wanasema wataalamu

Matokeo ya majaribio yanaonesha kuwa watu ambao wamepata dozi mbili za AstraZeneca wangeweza kuwa na kinga yenye nguvu kama wangepatiwa chanjo tofauti kama nyongeza.

Naibu Afisa Mkuu wa kitabibu nchini Uingereza, Prof Jonathan Van-Tam, amesema hakukuwa na sababu ya kubadili dozi za sasa za chanjo zinazoonesha mafanikio nchini humo, zikiwa zinapatikana vyema na kuokoa maisha.

Lakini anasema inaweza kuwa kitu cha kuangalia katika siku zijazo: "Kuchanganya dozi kunaweza kutupa mabadiliko zaidi kwa programu ya nyongeza, wakati pia ikisaidia nchi ambazo zinaendelea zaidi na utoaji wao wa chanjo, na ambao wanaweza kuwa na shida za usambazaji . "

Baadhi ya nchi tayari zinaztumia dozi mchanganyiko. Uhispania na Ujerumani wanatumia Pfizer au Mordena ya mRNA kama dozi ya pili kwa vijana ambao tayari walishapata dozi ya chanjo ya AstraZeneca, kutokana athari za kuganda kwa damu zaidi kuliko ufanisi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...