Search This Blog

Monday, June 28, 2021

Uhamasishaji wananchi kwenye miradi ya upanuzi IIA (DENSIFICATION IIA) yaendelea Tabora


Timu ya wataalamu wa Tanesco kitengo cha masoko makao makuu ikishirikiana na ofisa huduma kwa wateja mkoa wa Tabora  umeendelea na zoezi la uhamasishaji wa wananchi kwenye miradi inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini REA kupitia mkandarasi wa umeme kampuni ya Sengerema Electrica group (SEGL) ili kuandaa wananchi kuanza maandalizi ya wiring kwenye  nyumba zao mkoani Tabora.

Pamoja na kuanza maaandalizi ya utandazaji wa miundombinu ya umeme kwenye nyumba  pia wananchi hao wamepata fursa ya kujifunza maswala mbali mbali yanayohusu taratibu za kufuata ili kujiunganishia huduma ya umeme, Gharama ya kuunganisha umeme, wigo wa mradi kwenye maeneo yao, matumizi ya UMETA na umuhimu wa kutunza miundombinu ya shirika ikiwemo tahadhari ya kuchoma moto hovyo hasa  wakati wa kiangazi.

Wanchi pia wamepata fursa ya kuuliza na kupata elimu mbalimbali zinazohusiana na huduma za ki-Tanesco kama vile makundi ya matumizi ya wateja, adha iliyojitkeza  ya manunuzi ya LUKU kwa siku za karibuni, na hali ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo yao.

Wananchi wa maeneo mengi bado wameendelea kulalamikia wigo mdogo wa mtandao wa miundombinu ya umeme kwenye maeneo huku wakisisitiza kuwa hata miradi ya upanuzi bado haiwezi kutatua mahitaji yao kwani maeneo mengi bado yameachwa.

Zoezi la uhamasishji unaendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa Tabora(Sikonge, Urambo, Kaliua, Uyui, Nzega na Igung) isipokuwa Tabora manispaa ambayo haijanufaika na mradi wa  upanuzi IIA(Densification IIA).



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...