Ufaransa imesitisha operesheni za pamoja za kijeshi na Mali juu ya mapinduzi ya wiki iliyopita katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Ilisema ushirikiano wowote utasitishwa hadi itakapopata hakikisho kuhusu kurudi kwa utawala wa kiraia nchini Mali.
Vikosi vya Ufaransa vimekuwa vikisaidia wanajeshi kutoka Mali, Chad, Mauritania, Niger, na Burkina Faso kupambana na wanamgambo katika eneo la Sahel.
Mnamo Mei 25, mwanajeshi mwenye nguvu za kijeshi wa Mali, Col Assimi Goïta, alimwondoa mamlakani rais wa kiraia wa nchi hiyo
Wiki hii kundi la Afrika Magharibi la Ecowas na Umoja wa Afrika (AU) ziliibvua Mali unachama wa makudi hayo
Siku ya Alhamisi wizara ya majeshi ya Ufaransa ilisema kwamba Ecowas na AU wameweka "mfumo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Mali".
Iliongeza: "Wakati inasubiri hakikisho la kurejea kwa utawala wa kiraia , Ufaransa imeamua kusimamisha, kama hatua ya muda, operesheni za kijeshi za pamoja na vikosi vya Mali."
Vikosi vya Ufaransa vitaendelea kufanya kazi huko kwa njia huru
Assimi Goïta anayehudumu kama makamu wa rais amesema hakushauriwa kuhusu mabadiliko katika baraza la mawaziri
Kiongozi wa mapinduzi Kanali Assimi Goïta aliteuliwa kama rais wa mpito na korti ya katiba Ijumaa iliyopita - siku mbili baada ya kujitangaza kuwa kiongozi wa mpito.
Alitetea kuondolewa kwa Rais Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane kama hatua iliyohitajika kwa sababu walishindwa katika majukumu yao na walikuwa wakitafuta kuhujumu mabadiliko ya nchi.
Askari waliwakamata na kuwaweka kizuizini wanaume hao wawili baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri ambayo Kanali Goita alisema hakushauriwa juu yake.
No comments:
Post a Comment