MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imewataka watafiti sekta za mbalimbali nchini ikiwemo, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Afya, Ujenzi na kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuepusha maafa au madhara mbalimbali yanayojitokeza katika vipindi mbalimbali ambavyobkunatokea mabadiliko ya hali ya hewa
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa wa TMA Dk Ladisilaus Chang’a ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akitoa mada kwa wataalam wa sekta ya Afya, Kilimo na Mifugo kwenye warsha ya siku 4 iliondaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH.
Dk. chang'a amesema wataalam wa sekta hizo zote wakiwemo wananchi wanapaswa kuwa mstari wa mbele kusikiliza taarifa za TMA ambazo zinaweza kuwapa muongozo wa kuendesha Kilimo bila ya kupata hasara yoyote.
“Tunaomba mjenge utaratibu wa kutumia taarifa za TMA kwa sababu itawasaidia kuepuka hasara mbalimbali zinazojitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,”amesema
Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusabisha masuala ya Ukame katika maeneo tofauti, hivyo kama watafiti watatumia taarifa za TMA basi itawasaidia kufanya utafiti sahihi na kutoa taarifa ya eneo husika linapaswa kulima mazao gani ili yaweze kustawi.
Akizungumzia sekta ya Kilimo amesema wanapaswa kutumia taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa hususani katika utekelezaji wa shughuli za sekta ya Kilimo nchini ili kuepuka kutokea hasara kwa wakulima kwenye mazao wanayolima katika msimu husika.
Kwa upande wa sekta ya afya alisema mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kwa jamii lakini pia ongezeko la joto linaweza kuleta athari ya magonjwa kwa wananchi.
Dk.Chang'a amesema upande wa Mifugo pia mabadiliko ya hali ya hewa yanayoaeza kuleta athari kubwa kutoka na kusababisha ukame utakaopelekea Mifugo kukosa malisho na kufa, pia yanaweza kusababisha mafuriko ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya mifugo.
Akizungumzia suala la Ujenzi wa madaraja amesena nao inabidi wazingatie taarifa za hali ya hewa ili kuepuka kutokea kwa maafa pindi wanapoendelea na ujenzi
Naye Dk Goodluck Massawe Mhadhiri wa Sera Mipango na Menejimenti Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) amesema utafiti ni jambo zuri sana kuzingatiwa kwa sababu linasaidia jamii kuweza kufanya vitu kwa usahihi kulingana na matokeo chanya ya utafiti.
Masawe ametoa wito kwa wanasiasa kujenga utaratibu wa kutumia matokeo ya watafiti ili kuzungmza na wananchi wanaowaongoza katika
masuala mazima ya Kilimo.
No comments:
Post a Comment