Search This Blog

Monday, June 7, 2021

Tetes za soka kmatafa


 Manchester United wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili Jadon Sancho, 21, kutoka Borussia Dortmund baada ya bei ya winga huyo wa Uingereza kushuka hadi £80m. (Times)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo wa kati wa Villa na England Jack Grealish, 25, msimu huu. (ESPN)

Mshambuliaji wa Ureno Ronaldo, 36, anaelekeza darubini yake kwengine licha ya kufanya mazungumzo na Juventus kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (ESPN)

Endapo Ronaldo atahama Juve, Mbrazil Gabriel Jesus ,24, wa Manchester City anapigiwa upatu kuongoza katika orodha ya wachezaji watakaochukua nafasi yake. Wengine ni mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia, Dusan Vlahovic, 21, na Muargentina Mauro Icardi, 28, wa Paris St-Germainy. (Gazzetta dello Sport - kwa Kitaliano)

Everton wamemhoji kocha wa zamani wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47, kuhusu uwezekano wa kumrithi Carlo Ancelotti kama meneja wa klabu hiyo baada ya Mtaliano huyo kujiunga tena na Real 

Chelsea wameongeza juhudi za kumsaka mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund,"wanaamini" watafanikiwa kumpata nyota huyo , kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Primia Mjerumani mwenzake Jan Aage Fjortoft. (Mail)

Hawa ndiyo washambuliaji bora zaidi duniani msimu huu

Atalanta wameweka bei ya £52m kumuuza mlinzi wa Argentina Cristian Romero. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 23- amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Tuttosport - kwa Kitaliano)

Leicester wamekubali uhamisho wa pauni milioni 15 na Celtic kwa mshambuliaji wa Ufaransa Odsonne Edouard, 23. (Sun)

Newcastle wanataka kumenyana na Southampton katika usajili wa kiungo wa kati wa Leicester Muingereza Hamza Choudhury, 23. (Football Insider)

Kocha wa Fulham Scott Parker huenda akaondoka klabu hiyo ili kuwa meneja wa Bournemouth. (Talksport)

West Ham na Aston Villa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Chris Wood, huku Everton wakimnyatia kiungo wa kimataifa wa New Zealand wakati wanasupobiri uteuzi wa meneja mpya. (Mirror)

West Ham wamefikia mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Mfaransa Pierre Ekwah,19. (Sky Sports)

Aston Villa wanapigiwa upatu kumsaini mlinzi wa kati Josh Feeney,16, kutoka Fleetwood msimu huu wa joto, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester United. (Mail)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...