Search This Blog

Thursday, June 24, 2021

TANROADS Kuwasha Taa barabara za Miji ya mkoa wa Manyara


Na John Walter-Manyara

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Manyara Bashiri Rwesingisa amesema jumla ya shilingi Milioni 446 zinatumika kuweka taa bara barani katika miji ya wilaya za mkoa huo ikiwa ni jitihada za kuendelea kuboresha bara bara wanazozisimamia.

Akizungumza na kituo hiki amesema taa hizo zinawekwa Babati mjini,Magugu,Mdori mizani, mji wa Katesh,mji wa Mbulu,mji mdogo wa Dongobesh na maeneo mengine.

Amesema pamoja na faida zingine nyingi lakini faida mbili kuu ambazo ni kuboresha usalama muda wa Usiku kwa kuwa kuna baadhi ya wahalifu hutumia giza kuwaibia watu pamoja huku Faida nyingine ikiwa ni kuwawezesha watu katika miji kuendelea kufanya kazi za uzalishaji muda wa ziada.

“Hii yote itaongeza mapato na makusanyo ya serikali nay a  mtu mmoja mmoja katika mkoa wetu wa Manyara”alisema Rwesingisa

Aidha ametoa wito kwa wananchi  kuzilinda taa hizo kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake ili kuondoa kasumba ya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu ya bara bara  hatua inayorudisha nyuma jitihada za serikali kuwafikishia wananchi huduma bora za kijamii.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...