Search This Blog

Monday, June 28, 2021

Serikali ya Ethiopia yasitisha mapigano Tigray huku TPLF ikisherehekea ushindi


Serikali ya Ethiopia imetangaza kusitisha mapigano Tigray - miezi nane baada ya Waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed kutuma majeshi yake kukabiliana na waasi .

Kundi la waasi la TPLF limedai kuuchukua mji wa Mekelle lakini serikali haijathibitisha kuupoteza mji huo .

Tangazo hilo limekuja huku watu wakiripoti kushuhudia kutoona makundi ya kijeshi katika mitaa ya mji wa Mekelle.

Pande zote mbili zinashutumiwa kufanya mauaji ya watu wengi na kukiuka haki za binadamu.

Zaidi ya watu milioni tano wana uhitaji wa haraka wa msaada wa chakula, Umoja wa Mataifa umesema watu 350,000 wanakabiliwa na njaa.

Jumatatu, taarifa zimeanza kueleza kuwa wapiganaji wa Tigray - ambao walifanya mashambulizi makubwa wiki iliyopita walilazimisha utawala wa mpito kutoka Mekelle.

Baadhi ya watu wa Mekelle wameiambia BBC kuwa wanasheherekea kuondoka kwa wanajeshi wa serikali kuu.

Mtu ambaye hakutaka kufahamika kutoka serikali ya mpito ameiambia AFP kuwa"kila mtu ameondoka ", wakati mashahidi wawili wameiambia Reuters kuwa wanajeshi wa Tigray walikuwa wanaonekana Mekelle.

Lakini imetuma taarifa Jumatatu kufafanua suala la kusitisha mapigano mpaka msimu wa kilimo uishe na vilevile kuruhusu wale wenye uhitaji wa kuweza kufikiwa na vilevile kutoa muda ili wanasiasa wapate suluhu ya mgogoro huo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres, ambaye alizungumza na bwana Abiy siku ya Jumatatu , alisema wananchi wanalindwa , misaada ya kibinadamu , misaada ya kibinadamu inawafikia wananchi wanaohitaji na suluhu la kisiasa limepatika". Hatahivyo anategemea kuwa mapigano yataweza kusitishwa.

Katika siku ambayo mambo yalikuwa yanaenda haraka, wawakilishi wa serikali waliripotiwa waliripotiwa kuwa walikuwa wanapepea bendera kutoka Mekelle - na sio lazima Amani.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto Unicef imetoa taarifa kulaani kitendo cha askari wa taifa la Ethiopia, ambao wanasema waliingia katika ofisi yao na kuharibu vifaa vyao vya satelaiti.

Chanzo cha habari huko Mekelle kimeiambia BBC kuwa watu wanasheherekea katika mitaa na kwenye mitandao ya kijamii kuonesha wafuasi wa waasi wa Tigray walitembea kwa gwaride huku wamebeba bendera.

Mwezi Novemba mwaka jana serikali ya Ethiopia ilitangaza kufanya mashambulizi kwa waasi wa waliokuwa chama tawala , the Tigray People's Liberation Front (TPLF).

Chama hicho kilikuwa na wafuasi wengi kilitofautiana na waziri mkuu Abiy Ahmed juu ya mabadiliko ya kisiasa katika taifa ambalo linategemea mfumo wa shirikisho m - ingawa pia TPLF ilivamia ngome ya jeshi Tigray.

Bwana Abiy, ambaye ni mshindi wa tuzo za Amani za Nobel alitangaza kuwa mgogoro umeisha mwishoni mwa Novemba lakini mapigano yalikuwa yanaendelea.

Maelfu ya watu waliuawa. Makumi maelfu walikimbia makazi yao na kuwa wakimbizi nchi jirani ya Sudan.

Pande zote mbili zinashutumiwa kukiuka haki za binadamu.

TPLF iliungana na kikundi kingine cha wapiganaji Tigray na kutengeneza jeshi la ulinzi Tigray.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...