Raia wa jimbo lililojitenga la Somaliland wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa Bunge na Serikali za Mitaa uliofanyika jana ambao unatajwa kuwa mfano katika kanda ya pembe ya Afrika inayoandamwa na mizozo ya kisiasa.
Matokeo yanatarijiwa kuanza kutolewa leo na kuendelea hadi ndani ya muda wa siku tano baada ya zoezi la kupiga kura kufanyika kwa amani na utulivu kwenye jimbo hilo ambalo lilijitenga na Somalia na mwaka 1991 na kisha kujitangazia uhuru wake.
Zaidi ya watu milioni moja waliandikishwa kushiriki uchaguzi huo uliocheleshwa ambao unatajwa kuwa alama muhimu kwa demokrasia ya Somaliland.
Kwa miaka mingi eneo hilo ambalo bado halitambuliwi kuwa taifa huru limeshuhudia utulivu wa kisiasa tofauti na nchi nyingi za Pembe ya Afrika.

No comments:
Post a Comment