Search This Blog

Saturday, June 5, 2021

Putin aishtumu Marekani siku moja kabla ya mkutano na Biden


Rais wa Urusi Vladmir Putin hapo jana Ijumaa alitumia kauli kali kuzungumzia mkutano wake wa kesho na Rais wa Marekani Joe Biden, akiishtumu Marekani kwa kujaribu kuikandamiza Urusi.

 Akizungumza wakati wa mkutano wa kiuchumi mjini St. Petersburg, Putin alisema kuwa udhibiti wa silaha, mizozo ya ulimwengu, janga la virusi vya corona na mabadiliko ya tabianchi ni kati ya maswala watakayojadiliana na Biden wakati wa mkutano huo utakaofanyika mjini Geneva, Uswisi.

 Akitumia tukio la uvamizi wa Bunge la Marekani mnamo tarehe 6 Januari mwaka huu kulikofanywa na wafuasi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Donald Trump, kama ishara ya undumilakuwili wa mataifa ya Magharibi, alisema wavamizi hawakuwa wezi wala majambazi, bali watu wenye matakwa ya kisiasa, ambayo hayakusikilizwa.

 Hata hivyo, rais huyo wa Urusi amesema nchi zao mbili zinahitaji kutafuta njia za kurekebisha uhusiano wao uliodhoofika kwa sasa, huku akielezea matumaini kwamba mkutano huo utapunguza mvutano ulioko kati ya mataifa hayo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...