Search This Blog

Tuesday, June 1, 2021

Netanyahu asisitiza msimamo wake dhidi ya Iran


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa hawatojali kuhatarisha uhasama na Marekani katika kuzuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.

Netanyahu alifanya tathmini kwenye ajenda wakati wa sherehe iliyofanyika kufuatia uteuzi wa David Barnea katika nafasi ya Mkuu wa Huduma ya Ujasusi ya Israel (MOSSAD).

Akiteta kuwa tishio kubwa linalowakabili Israel ni uwezekano wa Iran kupata silaha za nyuklia, Netanyahu alitoa wito wa kuendelezwa kwa operesheni za siri dhidi ya Iran.

Akibainisha kuwa aliwasilisha maoni yake juu ya mpango wa nyuklia wa Iran kwa Rais wa Marekani Joe Biden, Netanyahu alisema,

"Nilimwambia hivi Joe Biden, ambaye amekuwa rafiki yangu kwa miaka 40: Makubaliano yawepo au yasiwepo, tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuizuia Iran isitengeneze nyuklia. Chaguo moja lipo kati ya mvutano wa uhusiano na Marekani ambayo ni rafiki zetu wakubwa, au kuondoa tishio lililopo. Ikiwa tutalazimika kuchagua njia ya mvutano ili kuondoa tishio, basi itakuwa hivyo."




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...