Search This Blog

Monday, June 7, 2021

Netanyahu adai udanganyifu wa uchaguzi wa Israel

 


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema muungano mpya ulioundwa karibuni ambao unalenga kumuondoa madarakani ni matokeo ya kile alichokiita kuwa ni udanganyifu mkubwa wa uchaguzi katika historia ya demokrasia. 


Saa chache baada ya kauli za Netanyahu, Naftali Bennett, kiongozi wa siasa kali za kizalendo anayetarajiwa kumrithi kama waziri mkuu, akamtaka kiongozi huyo aliyehudumu kwa muda mrefu kutowacha nyuma ardhi iliyowaka, na kukubali kuwa watu wanaruhusiwa kuunda serikali hata kama haitaongozwa na Netanyahu. 


Tuhuma za Netanyahu ambaye ni kiongozi wa chama cha Likud, zimekuja wakati mkuu wa usalama wa taifa akionya hadharani kuhusu uwezekano wa kuzuka vurugu. Hakuna tarehe iliyotangazwa ya kupigwa kura bungeni kuiidhinisha serikali mpya ya mseto.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...