Search This Blog

Sunday, June 13, 2021

Naibu Waziri Chande afanya ziara kiwanda cha A TO Z cha Arusha, Atoa maagizo mazito

 


Kiwanda cha A TO Z kimeelekezwa kuwa na utaratibu wa kuwasilisha katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingra (NEMC) ripoti ya vipimo vya sampuli ya majitaka ili liweze kufanya tathmini kuhusu kiasi cha sumu kinachoweza kuwemo katika maji hayo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande ametoa maelekezo hayo Juni 12, 2021 alipofanya ziara ya kukagua kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha.


Chande alibaini kuwa ripoti inayoandaliwa na wataalamu wa maabara kiwandani hapo huishia kuwasilisha kwa uongozi wa kiwanda pekee bila kuishirikisha Serikali ili wawafanyie tathmini.

“Nimetembelea kiwanda hiki na nimefika kule maabara nimebaini changamoto hasa katika ripoti zenu zinaishia humu ndani, ni sawa na kufanya mtihani halafu ukajisahihishia mwenyewe huwezi kufeli lazima mpeleke ripoti NEMC wawatahmini,” alisema.

Naibu waziri huyo alisema ipo haja ya kiwanda hicho kuwashirikisha wataalamu kutoka Wakala wa Mkemia Mkuu ili kuweza kupata uhakika wa matokeo ya vipimo kama ni sahihi.


Pia aliuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kutanua mtambo wa kutibu majitaka akibainisha kuwa ni mdogo ukilinganisha ukubwa wa kiwanda hali inayoweza kusababisha kushindwa kutosheleza mahitaji.

Hata hivyo Chande alipongeza kiwanda cha A TO Z kwa kushiriki katika utunzaji wa mazingira kutokana na ukusanyaji na urejelezaji wa taka unaofanywa kiwandani hapo.

Alisema kuwa hatua ya kukusanya taka mbalimbali husaidia kuweka Jiji la Arusha na nchi kwa ujumla katika hali ya usafi na kutunza mazingira na kuwataka wananchi waendelee kutunza mazingira kwani ndio uhai.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...