Shughuli za kujenga upya nyumba zilizoharibiwa zitachukua mieziImage caption: Shughuli za kujenga upya nyumba zilizoharibiwa zitachukua miezi
Karibu watu 500,000 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameachwa bila maji safi ya kunywa baada ya mlipuko wa volkeno wiki mbili zilizopita Shirika la Médecins Sans Frontières (MSF) limeonya.
Shirika hilo limesema kuwa ugonjwa wa kuhara ni janga na umekuwa tishio kubwa hivyo basi, kuna haja ya kuhakikisha watu wa mji wa Goma wamepata maji safi ya kunywa.
Hifadhi na mabomba yaliharibiwa pale mlima Nyiragongo ulipolipuka Mei 22.
Aidha, mamia ya maelfu ya watu bado hawajaweza kurejea katika nyumba zao.
"Tunasaidia kutoa mahitaji ya dharura kwa watu waliolazimika kuhama makazi yao, lakini haitoshi," amesema Magali Roudaun, mkuu wa MSF anayeongoza shughuli za utoaji msaada huko DRC.
"Tunahitaji msaada wa dharura kutoka kwa mashirika mengine ya kutoa misaada ili kusaidia watu."
Shirika la MSF limesema timu yake ilikuwa inatoa huduma za matibabu katika mji uliokaribu wa Sake, "ambapo kati ya watu 100,000 na 180,000 wamekusanyika makanisani, shuleni, misikitini na mitaani".
Mlima Nyiragongo, kilomita 10 (maili sita) kutoka mji wa Goma, ulilipuka na kusababisha mtirirko lava siku 10 zilizopita, na kupelekea mauaji ya watu 32, UN imesema.
Kumekuwa na mitetemeko mingi nchini humo tangu tukio hilo .
Katika juhudi za kutathmini kiwango cha hatari, wataalam wamepeleka ndege zisizokuwa na rubani katika kreta inayofuka moshi ambapo lava inayoyeyuka imekuwa ikimwagika.

No comments:
Post a Comment