NA THABIT MADAI, ZANZIBAR.
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema kwa kipindi cha miezi nane ya Uongozi wake ndani ya Mkoa huo amefanikiwa kuimarisha nidhamu, Uadilifu pamoja na uwajibikaji wa wafanya kazi wa tasisi za Umma Mkoa humo.
Amesem mafanikio mengine ni pamoja na kusimamia na kutekelea kwa vitenndo maagizo 13 waliyopatiwa na Rais wa Zanzibar Dk Husein Ali Mwinyi wakati wanapoapishwa kuwa wakuu wa mikoa.
Hayo ameyaeleza wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Tunguu, alisema kuwa moja ya changamoto iliyokuwa inarudisha nyuma maendeleo nda ya mkoa huo ni pamoja na wafanyakazi wa taasisi za umma kutokuwa na nidhani,Uadilifu pamoja na uwaibikaji kazini.
Alisema mafanikio mengine yaliyopatikana kwa kipindi cha miezi nane ni kusimamia vyema miradi mbaimbali ya meendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo sambamba na kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wnanchi mkoa humo.
“Kwa kipindi ifupi ukweli kuwa tumepata mafanikio mengi ikiwemo kusimamia miradi mbaimbali ya maedeleo pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wetu,”alisema.
Alieleza kuwa, Migogoro ya ardhi katika mkoa huo ni moja ya changamto ilikuwa inawasumba wananchi kwa kipindi kirefu.
“Migogoro ya ardhi ni jambo kubwa inalowakabili wananchi ndani ya mkoa wa Kusini ila kwa kipindi kifupi jumla ya kesi 125 tulizipokea na 43 tulizitolea maamuzi kwa ngazi ya mkoa na wilaya zetu n kesi zilizobaki zilikuwa katika hatua ya mahakama hivyo hatukuweza kuingilia mahakama,” alieleza.
Aidha alieleza kwamba ndani ya kipindi hicho alihakikisha anatekeleza majukumu yake ya msingi huku akizingatia maagizo 13 waliyopatiwa na Rais wakati wa kula kiapo kutumikia wananachi.
“Tulipoapishwa kuwa wakuu wa mikoa mwezi Novemba mwaka jana tulipewa maagizo ya Mhe, Rais kwenda kuyatekeleza hivyo hadi kufikia leo takribani mambo kadhaa tayari nmeshayatekelea na kuona mafanikio yake,” alieleza.
Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Mkoa alibainisha kwamba ukusanyaji wa mapato ndani ya Mkoa huo umeimarika kutoka shilingi Milion 895 mwaka jana na kufikia zaidi ya Bilion 1.2 kwa mwaka huu.
Hata hivyo Rashid Hadid Rashid alisema kwamba wamefaniiwa kutunza hali ya Amani na usalama ndani ya Mkoa huo ambapo raia bado wanaishi katika utii washeria na kanuni mbalimbali za nchi.
Katika hatua nyingine alibainisha kwamba mkoa tayari umeshatenga maeneo ya biashara na kilimo kwa vijana mbalimbali mkoani humo.
“Katika kuwainua vijana wetu tayari tueshatenga eneo la biashara pamoja na kilimo kwa vijana wetu ambao lengo ni kuwainua kimaisha na wasiwe tegemezi,”alibainisha.

No comments:
Post a Comment