Search This Blog

Wednesday, June 9, 2021

Mjumbe wa ECOWAS awasili Mali kwa mazungumzo na Goita


Mjumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi - ECOWAS Goodluck Jonathan amewasili Mali jana, siku moja baada ya Kanali Assimi Goita kuahidi kuirejesha haraka nchi hiyo mikononi mwa utawala wa kiraia baada ya kuongoza mapinduzi ya pili ya kijeshi katika miezi tisa.

 Jonathan, rais wa zamani wa Nigeria, anayewakilisha ECOWAS yenye mataifa 15 wanachama, anakutana na Goita ili kuuzungumzia mustakabali wa nchi hiyo. 

ECOWAS ilisitisha uwanachama wa Mali kufuatia mapinduzi ya pili ya kijeshi lakini haikuiwekea vikwazo vipya baada ya kufanya hivyo wakati wa mapinduzi ya kwanza. 

Katika hotuba yake ya kuapishwa Jumatatu wiki hii, Goita aliahidi kuwa Mali itatekeleza ahadi zake zote na kusema ataheshimu muda wa kuandaliwa uchaguzi uliowekwa na serikali ya mpito.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...