Search This Blog

Wednesday, June 23, 2021

Magereza yaeleza sababu za kufanikiwa kuanza kujitegemea kwa chakula


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema Siri ya mafanikio kwa jeshi hilo kuwa ni kujituma, kutokaka kwenye utendaji kazi wa mazoea na kudhamiria kuondokana na tegemezi ambapo wameanza Ujenzi wa nyumba 300 katika magereza zote nchini kwa ajili ya makazi ya maofisa na askari.

Pia amesema kati ya nyumba hizo 300 nyumba 100 zitajengwa makao makuu ya nchi Dodoma na kwamba mbali na hizo tayari wanakamilisha Ujenzi wa nyumba zaidi ya 20 katika Ofisi magereza ya Msalato na Isanga jijini hapa.

Meja Jenerali Mzee ameeleza mafanikio hayo jijini Dodoma wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya nchi Ulinzi na Usalama ya kutembelea Ofisi ya Magereza Msalato na Gereza la Isanga ziara iliyoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachaweni.

Amesema Rais, Hayati John Magufuli aliwapatia fedha sh. bilioni mbili ili ziwawezeshe kuboresha magereza hapa nchini, waliamua kutumia fedha hizo Kujenga karakana ya kuzalisha na kuuzia thamani mbalimbali ambacho tayari kimekamilika na kimeanza uzalishaji kikitarajiwa kuzinduliwa wakati wowote kuanzia sasa kitakachotengeneza bidhaa bora na za Bei nafuu.

Kuhusu makazi Kamishna huyo amefafanua kuwa mbali na Ujenzi huo waliamua kutumia fedha hizo kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba za zaidi ya 20 makazi ya maofisa na Askari ambao walikuwa wakiishi katika mazingira yasiyo salama sana.

Akizungumzia Ujenzi wa nyumba 300 unaoendelea, amesema waliongezewa fedha na Rais, Hayati Magufuli ambapo wametenda kiasi cha sh.bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo ambapo nyumba 100 zitajenga Dodoma huku nyumba 200 zikijengwa kwa mgawanyo katika magereza zote nchini zilizobakia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...