Search This Blog

Wednesday, June 9, 2021

Kumbilamoto atoa msaada katika kituo cha yatima Zingiziwa


Meya Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto kwa kushirikiana na Taasisi ya HOT inayoongozwa na Mwenyekiti wake Bi Angela Mwasha wamekabidhi msaada wa Chakula katika Kituo cha kulelea Watoto Yatima kilichopo katika Kata ya Zingiziwa, Halfa ya Makabidhiano imefanyika katika Kituo hicho kilichopo katika Kata ya Zingiziwa Mtaa wa Zingiziwa.

Taasisi ya HOT nimiongoni mwa Taasisi ambazo zilizoweza kupata Mkopo unaotolewa na Halmashauri ya Jiji ambapo waliweza kuutumia Mkopo huwo kama sehemu ya mtaji kwao na kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi za mikono ikiwemo kutengeneza batiki.

Mhe. Kumbilamoto amewapongeza Taasisi hiyo ya HOT kwa kuwa ni miongoni mwa Taasisi za mfano ambazo ziliwezeshwa na Halmashauri ya Jiji na hatmaye kurudisha fadhira kwa kutoa misaada hasa kwa watu wenye huitaji.

Bi. Angela Mwasha amesema kuwa Taasisi ya HOT inajishughulisha na utengenezaji wa Batiki lakini pia ameishukuru Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa kuwawesha kupata mkopo ili kuinua Taasisi yao. Lakini pia ameeleza vitu ambavyo walitoa kama msaada katika kituo hicho ikiwemo Mchele, Mafuta ya kipitia, Maharage, Unga wa ngano, Unga wa Sembe, Sukari pamoja na Sabuni.

Aidha kwa upande wa Diwani wa Kata y Zingiziwa Mhe. Maige Maganga ametoa shukrani zake za dhati kwa Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto pamoja na Taasisi ya HOT kwa kuichagua Zingiziwa kwani zipo Kata nyingi katika Jiji ila Msaada huwo ukaletwa Zingiziwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...