Search This Blog

Monday, June 21, 2021

Kuleba ahimiza kujiunga na muungano wa NATO


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmitro Kuleba alikumbusha katika mkutano wa mwisho wa NATO kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano na kusema,

"Swali langu kwa NATO ni kwamba mnataka mageuzi mangapi? Tunaomba mtupe orodha ya wazi."

Kuleba, ambaye yuko jijini kuhudhuria Mkutano wa Diplomasia wa Antalya, alisisitiza kwamba lugha inayowakilisha kujitolea kwa kisiasa ilitumika katika vikao viwili kuhusu mkutano wa NATO na G7 iliofanyika wiki iliyopita.

"Kwa hivyo lugha hii inakidhi matarajio yetu tunapofafanua jukumu la kweli kwamba ni kuunga mkono mapambano ya Ukraine ya enzi kuu juu ya uadilifu wake wa eneo na jukumu la uharibifu la Urusi katika kanda." Kuleba alitoa maelezo hayo.

Kuleba pia alikumbusha kwamba NATO ilirudia ahadi yake ya kisiasa mnamo 2008 katika mkutano wa mwisho na ilitangaza kuwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano huo.

Dmitro Kuleba aliongezea kusema,

"Kwa kweli, hatujali ni namna gani tunaweza kuingia katika NATO maadamu tunajua kuna dhamira ya kisiasa na ratiba ya kufikia lengo hilo."

Kuhusu mambo ya kufanywa katika mchakato wa kujiunga na NATO, Kuleba alisema,

"Swali langu kwa NATO ni kwamba mnataka mageuzi mangapi? Tunaomba mtupe orodha ya wazi."

Kuleba alielezea kuwa ingawa Rais wa Marekani Joe Biden alisisitiza kwamba Ukraine itajumuishwa katika NATO kwenye hotuba zake nyingi, hawakupewa kidokezo hata kimoja kuhusu ratiba ya nyakati.

Kwa upande mwingine, akizungumzia ununuzi wao wa vyombo vya angani visivyo na rubani (SİHA) kutoka Uturuki, Kuleba alifahamisha kwamba wanataka kujumuisha SİHA hizo injini za Kiukreni na kuzanisha uzalishaji wa SİHA na kwamba wanafanya kazi na upande wa Uturuki katika suala hili.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...