Search This Blog

Wednesday, June 23, 2021

Kikosi cha Azam kwenda songea leo kuivutia kasi Simba

 


KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina,  leo Juni 23 kinaanza safari kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.

Mchezo huo wa hatua ya nusu fainali unatarajiwa kuchezwa Juni 26, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Kikosi hicho kinaondoka na ndege, Uwanja wa Julius Nyerere. Ikumbukwe kwamba mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambao utawakutanisha Biashara United v Yanga.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanaamini kwamba watapata ushindi.

Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambapo walitwaa msimu uliopita kwa kushinda mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa fainali.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...