Search This Blog

Saturday, June 5, 2021

Kamanda Magiligimba ahamishiwa Ilala


Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Makamanda watatu wa Polisi wa mikoa ya Ilala, Shinyanga na Songwe.

Katika mabadiliko hayo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) ACP Debora Magiligimba aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga amehamishiwa Mkoa wa Kipolisi Ilala Kanda Maalumu ya Dar es salaam,akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Janeth Magomi anayeenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe.

Katika Mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), George Kyando aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...