Jumuiya ya Ulaya (EU) imeamua kuongeza vizuizi vya kiuchumi dhidi ya Urusi kwa miezi mingine 6 kwa madai kwamba inaonea Ukraine.
Akichapisha kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii baada ya Mkutano wa Viongozi wa EU uliofanyika Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji, Rais wa Baraza la EU Charles Michel alisema kuwa iliamuliwa kuongeza vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na EU kutokana na Urusi kuidhoofisha Ukraine.
Michel amebaini kuwa Urusi lazima ichukue jukumu lake kuhakikisha utekelezaji kamili wa Mkataba wa Minsk.
Akiashiria kwamba EU itafuata kanuni inayotegemea usawa na mkakati kuhusu Urusi, Michel alisema, "Tumeongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi."
Kulingana na uamuzi huo, vikwazo dhidi ya Urusi vitaongezwa hadi Januari 31, 2022.

No comments:
Post a Comment