Polisi wa Israel waliingilia kati maandamano ili kukabiliana na waandamanaji waliounga mkono Wapalestina katika Wilaya ya Sheikh Jarrah.
Wakijaribu kumzuia mpiga picha wa Al Jazeera ambaye alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa kuchukua filamu, polisi pia walimnyooshea bunduki mwanahabari wa kike wa Al Jazeera, Givara Budeiri, ambaye alipingana nao na kumzuia.
Kamera za timu ya Al Jazeera pia ziliharibiwa katika makabiliano hayo.
Wakitishia waandamanaji kwa kutumia nguvu, polisi wa Israel waliwatawanya waandamanaji na kuchukua bendera zao.
Al Jazeera ililaani shambulizi la polisi wa Israel dhidi ya wafanyikazi wa kituo hicho.
Kikielezea shambulizi hilo kuwa kama la "kustaajabisha", kituo hicho cha utangazaji kilisema, "Hii ni sura mpya katika safu ya mashambulizi ya Israel." Litoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa waandishi wote.
Pia kiliitaka jamii ya kimataifa, vyombo vya habari na mashirika ya haki za binadamu kulaani vitendo vya serikali ya Israel.
Wakati huo huo, mwandishi aliyezuiliwa Givara Budeiri aliachiliwa. Walakini, mamlaka ya Israel iliamua kumpiga marufuku Budeyri kuingia katika Wilaya ya Sheikh Jarrah ya Jerusalem kwa siku 15.
Katika mashambulizi yaliyozinduliwa na Israel kwenye Ukanda wa Gaza uliozingirwa mnamo Mei 10, ndege za kivita zililenga jengo hilo, pamoja na ofisi za Associated Press na Al Jazeera, na kuharibu jengo la ghorofa 13.

No comments:
Post a Comment