Serikali mpya ya muungano iliyoundwa chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Naftali Bennett huko Israel iliidhinisha mradi wa ujenzi wa majengo mapya 31 katika makazi haramu ya Wayahudi yaliyoko Ukingo wa Magharibi uliokaliwa.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, Kamati Ndogo ya Mipango ya Utawala wa Kiraia ilichunguza miradi ya ujenzi wa majengo 33 katika makazi haramu ya Wayahudi ya Ukingo wa Magharibi.
Baada ya uchunguzi, ujenzi wa majengo 31 mapya uliidhinishwa.
Miongoni mwa majengo yaliyoidhinishwa kwa ujenzi ni maduka makubwa na masinagogi 2.
Hivyo basi, serikali ya mseto inayoongozwa na Bennett, ambayo ilichukua madaraka mnamo Juni 13 kwa kura ya imani, iliidhinisha kwa mara ya kwanza miradi ya ujenzi katika makazi haramu ya Wayahudi ya Ukingo wa Magharibi.
Kuna zaidi ya makazi ya Wayahudi haramu 250 katika Ukingo wa Magharibi, ambayo Israel ilinyakuwa mwaka wa 1967.
Zaidi ya walowezi wa Kiyahudi 400,000 wanaoishi katika maeneo haya hufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa Wapalestina wanaoishi chini ya umiliki katika Ukingo wa Magharibi.
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, makazi yote ya Kiyahudi katika maeneo yaliyokaliwa yanachukuliwa kuwa haramu.

No comments:
Post a Comment