Search This Blog

Tuesday, June 8, 2021

Harris apeleka vita vya rushwa Guatemala na kuwaonya wahamiaji


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amesema amefanya mazungumzo mapana na Rais wa Guatemala Alejandro Giammattei kuhusu kupiga vita rushwa ili kuzuia uhamiaji kutoka Amerika ya Kati na akawaonya wazi wazi wahamiaji kutokwenda Marekani. 

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari pamoja na Giammattei, Harris amesema Marekani itaendelea kutekeleza sheria za kuhakikisha usalama wa mipaka yake huku akiwaambia wahamiaji kuwa watarudishwa walikotoka kama wataikaribia mipaka ya Marekani. 

Tangu Rais Joe Biden aingie madarakani, idadi ya wahamiaji wanaokamatwa kwa mwezi kwenye mpaka wa Marekani na Mexico imeongezeka kwa viwango vikubwa kabisa katika miaka 20. Harris, leo anatarajiwa kukutana na Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...