Search This Blog

Monday, June 7, 2021

Chama cha Merkel chashinda uchaguzi wa mwisho wa mkoa

 


Chama cha Kansela Angela Merkel wa Ujerumani cha Christian Democratic Union - CDU kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwisho wa mikoa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa kwanza katika miaka 16 bila kumhusisha kansela huyo mkongwe. Matokeo hayo yamempiga jeki atakayekuwa mrithi wake wa kihafidhina. 


Matokeo ya mapema yanaonyesha kuwa chama cha CDU chini ya kiongozi mpya Armin Laschet kimeshinda karibu asilimia 37 ya uchaguzi wa jimbo la Saxony-Anhalt, dhidi ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia AfD katika nafasi ya pili na asilimia 21. 


Chama cha Merkel kwa miaka mingi kimekuwa nguvu kubwa katika jimbo la Saxony-Anhalt la iliyokuwa Ujerumani Mashariki, kwa kushinda uchaguzi wote wa eneo hilo isipokuwa mmoja tu tangu kuungana kwa Ujerumani mbili mwaka wa 1990.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...