BAADA ya kwenda DR Congo na kumsainisha beki wa kulia wa AS Vita, Shabani Djuma, Injinia Hersi Said, amepaa na kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo imebainika kuwa anaenda kukamilisha usajili wa mshambuliaji anayekipiga katika ligi kuu nchini humo.
Hersi ambaye ni Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Jumatano alikwea pipa kwenda nchini Congo ambako alikamilisha usajili wa beki wa kulia Shabani Djuma kisha Alhamisi akapaa kuelekea nchini Afrika Kusini kukamilisha usajili wa mshambuliaji mwingine.
Chanzo chetu cha ndani kutoka nchini DR Congo kimeliambia Championi Ijumaa, kuwa ni kweli bosi wa Yanga alikutana na uongozi wa mchezaji Shabani Djuma katika hoteli ya kishua inayofahamika kwa jina la Fleuve Congo.
Hotel hiyo inayopatikana jijini Kinshasa nchini DR Congo ambapo bosi huyo baada ya kumalizana na Djuma, Alhamisi aliaga kuwa anakwenda Afrika Kusini kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine.
“Ni kweli kiongozi wa Yanga Jumatano usiku alionekana katika hoteli inayoitwa Fleuve Congo iliyopo jijini Kinshasa ambapo walikutana na uongozi wa Shabani Djuma na bosi huyo ambapo walikuwa wakikamilisha usajili wa mchezaji huyo,” kilisema chanzo hicho.

No comments:
Post a Comment