Zaidi ya watu 150 wamejeruhiwa usiku wa kuamkia leo katika ghasia zilizozuka wakati wa makabiliano baina ya Wapalestina na polisi wa Israel katika eneo la msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.
Maelfu ya waumini wa Kiislamu walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya swala ya ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati polisi wa Israel walipoimarisha ulinzi katika eneo la msikiti.
Katika wiki za hivi karibuni, Machafuko yameongezeka katika maeneo ya Ukingo wa Magharibu na Mashariki mwa Jerusalem, baada ya wapalestina kupinga vizuizi vya Israel katika maeneo ya mji wa zamani na pia uwezekano wa familia za Kipalestina kuondolewa kwenye makaazi yao kwa ajili ya kupisha walowezi.
Marekani imezitaka pande zote kupunguza mivutano huku Umoja wa Mataifa ukionya kwamba hatua hiyo inaweza kuheshabiwa kama uhalifu wa kivita.

No comments:
Post a Comment