Search This Blog

Sunday, May 2, 2021

Waziri Mkuu Majaliwa akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya kimataifa ya 29 ya kuhifadhi Quran Tukufu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mshindi wa kwanza wa kusoma Qur’an kwa njia ya tajweed kutoka Tanzania, Mohammed Harun  (kushoto) katika Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya Qur’an kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Mei 2, 2021.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Abubakar Kunenge, Wa pili kushoto ni  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir , wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuhifadhisha Quran, Shekh  Othman Kaporo na kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mshindi wa Kwanza  wa Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Kuhifadhi  Qur’an Tukufu kutoka Yemen, Mohammed Abdo Ahmed  (kushoto) hundi ya Dola za Marekani 5,000 katika fainali za mashindano hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Mei 2, 2021.  Kulia ni Mwenyekiti Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur’an, Sheikh  Othman Kaporo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Fainali za Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur’an kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Mei 2, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya waumin wa dini ya kiislaam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza katika Fainali za Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Kuhifadhi  Qur’an Tukufu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mei 2, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kukabidhi zawadi na kuzungumza katika Fainali za Mashindano ya  Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, Mei  2, 2021 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)





 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...