Search This Blog

Monday, May 24, 2021

Wabunge wapya uchaguzi mdogo waapishwa bungeni


 Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Jumatatu Mei 24, 2021  amewaapisha wabunge wawili waliochaguliwa hivi karibuni katika majimbo ya Mkoa wa Kigoma.

Wabunge hao ni Dk Florence Samizi wa jimbo la Muhambwe na Kavejuru Felix wa la Buhigwe,  wote wakitokea CCM.

Mbunge wa Buhigwe, Kavejuru Eliadory Felix akila kiapo cha uaminifu na utii bungeni mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Wabunge hao  wameapishwa baada ya  ushindi waliopata katika uchaguzi mdogo uliofanyika kwa majimbo hayo kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Muhambwe,  Atashasta Nditiye na Dk Philip Mpango wa Buhigwe aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Licha ya kusindikizwa na wabunge wengi,  hakukuwa na shamrashamra kubwa kama ambavyo imezoeleka katika uapisho wa wabunge wanaochaguliwa kwenye chaguzi ndogo



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...