Search This Blog

Friday, May 28, 2021

Urusi: Marekani haitarudi kwenye mkataba wa Open Skies


Rais wa Marekani Joe Biden ameijuulisha Urusi kwamba nchi yake haitarudi tena kwenye mkataba wa Open Skies unaoziruhusu nchi kurusha ndege kwenye anga za mataifa mengine kwa kutowa taarifa ya muda mfupi kwa lengo la kufuatilia shughuli za kijeshi. 

Biden amefanya uamuzi huo jana baada ya juzi Jumatano bunge la Urusi kuidhinisha rasimu ya sheria iliyowasilishwa na Rais Vladimir Putin ya kutaka kuiondoa nchi yake kwenye mkataba huo. 

Rais wa zamani Donald Trump aliamua kuiondoa Marekani kwenye mkataba huo wakati wa uongozi wake, lakini uamuzi wa Biden ulikuwa bado haijulikani kwa hakika na sasa umeamua kuendelea na msimamo wa utawala uliopita.

 Mkataba huo inasemekana kuwa nguzo ya uaminifu kati ya wanachama wa NATO na Urusi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...