Search This Blog

Wednesday, May 12, 2021

Umoja wa Ulaya waifungulia kesi nyingine AstraZeneca kwa kuchelewesha chanjo

 


Umoja wa Ulaya umefungua kesi yenye lengo la kuilazimisha kampuni ya dawa ya AstraZeneca kuhakikisha itawasilisha mamilioni ya dozi za chanjo dhidi ya COVID-19 ifikapo mwezi Julai. 

Kesi hiyo ni ya pili kufunguliwa na umoja huo dhidi ya kampuni hiyo ya dawa ya Uingereza na Sweden, kutokana na kuchelewesha usambazaji wa chanjo. 

Msemaji wa Umoja wa Ulaya amesema wanaitaka mahakama kuiagiza AstraZeneca kuwasilisha dozi za ziada milioni 90, ikiwa ni zaidi ya milioni 30 ambazo tayari ziliwasilishwa kwenye robo ya kwanza. 

Wakili wa kampuni hiyo amesema jana kwamba kesi hiyo haikuwa na msingi kwa kuwa tayari wako katikati ya kesi nyingine. 

AstraZeneca awali iliahidi kusambaza dozi milioni 300 kuanzia Disemba mwaka jana hadi Juni, lakini hadi sasa ni dozi milioni 50 tu zimewasilishwa.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...