Ujumbe amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umeagiza kuachiwa huru mara moja kwa Rais wa Mali Bah Ndaw na Waziri Mkuu Moctar Ouane, baada ya taarifa kuibuka kwamba wanazuiliwa na wanajeshi.
Katika ujumbe wa Twitter ulioandikwa kwa Kifaransa, Minusma pia imetoa wito wa utulivu katika taifa hilo masikini la Afrika Magharibi.
Kauli hiyo imetokana na ripoti kwamba Rais wa mpito Ndaw na Bw. Ouane walipelekwa na wanajeshi hadi kambi ya kijeshi ya Kati karibu na mji mkuu, Bamako.
Jumatatu jioni, Bw. Ouane aliliambia shirika la habari AFP kwa njia ya simu kwamba wanajeshi "walikuja kumchukua". Shirika hilo la habari baadaye ilisema mawasiliano ya simu baadaye yalikatizwa.
Ripoti ya kuzuiliwa kwa viongozi hao ilikujua saa kadhaa baada ya serikali kufanya mabadiliko ambayo yalipelekea kuondolewa kwa maafisa wawili wa ngazi ya juu jeshini waliohusika katika mapinduzi ya mwaka jana.
Kwa mara nyingine tena Mali inakabiliwa na hali ya msukosuko miezi tisatu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubakar Keïta.

No comments:
Post a Comment