Search This Blog

Saturday, May 29, 2021

Ulaya yaidhinisha chanjo ya BioNTech-Pfizer kwa watoto


Shirika la Kudhibiti Madawa barani Ulaya, EMA limetangaza kwamba limeidhinisha matumizi ya chanjo ya virusi vya corona ya BioNTech-Pfizer kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 15. 

Hiyo ni chanjo ya kwanza kuidhinishwa kwa watoto wa Umoja wa Ulaya. EMA imesema chanjo hiyo haina madhara kwa watoto. 

Ujerumani inatarajia kuanza kutoa chanjo hizo kwa watoto wa shule kuanzia Juni 7, baada ya mkutano kati ya Kansela Angela Merkel na wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani siku ya Alhamisi. 

Chanjo ya BioNTech-Pfizer kwa mara ya kwanza ilianza kutumika kwenye nchi za Umoja wa Ulaya mwezi Desemba. 

Tangu wakati huo, takriban dozi milioni 173 zimetolewa kwenye umoja huo. Marekani na Canada tayari zimeanza kutoa chanjo kwa watoto wenye umri wa miaka 12.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...