Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA leo limefungua uchunguzi wa kinidhamu dhidi ya klabu tatu za kandanda ambazo bado hazijatangaza kujitoa kwenye mpango wa kuanzisha ligi mpya.
Wajumbe wa kamati ya nidhamu na maadili ya UEFA wameteuliwa kuongoza uchunguzi juu ya iwapo klabu za Real Madrid, Barcelona na Jeventus zimekiuka muongozo wa kisheria wa UEFA kwa kuwa sehemu ya mpango wa kuanzisha Super League.
Klabu hizo tatu kati ya 12 zilizohusishwa na mipango ya kuanzishwa kwa Super League ndiyo pekee bado hazijatangaza kuachana na malengo ya kushiriki ligi hiyo.
Klabu zote sita zinazocheza ligi ya England pamoja na Atletico Madrid, Inter na AC Milan zilikwisharifu kujitenga na ligi hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa mashabiki, serikali na taasisi za soka.

No comments:
Post a Comment