Search This Blog

Sunday, May 16, 2021

Tumecheza hovyo na kufanya makosa, tumeadhibiwa - Manara

Baada ya dakika 90 kukamilika na ubao wa Uwanja wa FNB Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, Ofisa Habari wa Simba,  Haji Manara amesema kuwa walicheza hovyo.

Kichapo hicho kinakuwa cha kwanza kwa Kocha Mkuu Didier Gomes kushuhudia idadi kubwa ya mabao kwa timu yake ikifungwa akiwa katika benchi baada ya kupokea mikoba ya Sven Vandenbroeck.

Haji Manara kupitia Ukurasa wake wa Istagram alisema:" Alhamdulillah. Tumefungwa na aliye bora usiku wa leo, tumecheza hovyo na tumefanya makosa mengi yaliyostahili adhabu hii.

"Life go on, (maisha lazima yaendelee) na still, (bado) tunazo dk tisini nyingine za kuamua,".

Mchezo wa robo fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22 ambapo Simba wanapaswa kufunga mabao zaidi ya manne ili kusona mbele hatua ya nusu fainali.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...