Search This Blog

Sunday, May 30, 2021

Tetesi za Soka Ulaya leo 30.05.2021

Manchester United wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo huku klabu hiyo ya Italia ikiwa iko tayari kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa miaka 36 kwa kubadilishana na kiungo wa kati Paul Pogba , 28. (Gazzetta dello Sport via Express)


Tottenham wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus,24, ambapo itashuhudia kubadilishana na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane,27, pamoja na nyongeza ya fedha.(Star)

Kiungo wa kati Dani Ceballos, 24, amesema anataka kusalia Real Madrid msimu ujao au kuondoka kabisa kwenye klabu baada ya kutumia misimu miwili akichezea klabu ya Arsenal (Mail)

Burnley wamepanga kutoa zabuni ya pauni milioni 10 kwa ajili ya mlinzi wa kati Joe Worrall,24. (Sun)

Tottehnam wana mpango wa kuanza mazungumzo rasmi na Paris St-Germain siku ya Jumatatu ukiwa mpango wa kumrejesha Mauricio Pochettino kwenye klabu. (Sun)

Mshambuliaji wa Tottenham Steven Bergwijn anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa joto huku Ajax ikiwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo, 23.(De Telegraaf)

Aston villa wana hofu ya kumpoteza kiungo wao nyota Douglas Luiz ,23, huku timu yake ya zamani ya Manchester City ikihitaji kumsajili tena Mbrazili huyo.(90 Min)

AC Milan wataanza mazungumzo na Chelsea Jumatatu kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa England Fikayo Tomori,23 kwa mkataba wa kudumu. (Sport Witness)

Arsenal imemwambia kocha wa Roma Jose Mourinho kuwa wanahitaji pauni milioni 17 kwa ajili ya kiungo wa kati Granit Xhaka, 28. (Gazzetta dello Sport)

West Ham wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Mzambia Patson Daka wanapotafuta namna ya kuziba nafasi ya Sebastian Haller. Mchezaji huyo wa miaka 22 pia amevutiwa na Liverpool, Manchester United na Manchester City. (Zam Foot)

Leeds hawana mpango tena wa kumnyakua kiungo wa kati wa Liverpool Harry Wilson msimu huu wa joto. (Football Insider)

Mwenyekiti wa Brighton Tony Bloom yuko tayari kusikiliza ofa za wachezaji kama kiungo wa Mali Yves Bissouma, 24, na mlinzi wa Kiingereza Ben White, 23, huku wakizivutia Arsenal, Liverpool na Manchester United. (The Athletic)

Southampton wana mpango kumsajili kiungo wa Everton Tom Davies baada ya mwaka jana kushindwa kumsajili Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22.(Football Insider)

Mchezaji wa Manchester United Diogo Dalot amekiri kuwa hajui mustakabali wake baada ya kiungo huyo wa kati,22, kucheza kwa mkopo AC Milan msimu uliopita. (Manchester Evening News)

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...